BUNGE LA LIBYA LAVAMIWA
Wanamgambo waliojihami kwa
bunduki, wamekalia bunge la Libya,
kuelezea masikitiko yao
kuhusiana na jinsi serikali mpya ya nchi hiyo ilivyoundwa.
Wanamgambo hao wanataka baadhi ya mawaziri kuondolewa,
kwa sababu wanatuhumiwa kuwa na uhusiano na rais wa zamani wa nchi hiyo Muammar Gaddafi.
Malori kadhaa, yakiwa yamesheheni silaha za kutungulia ndege zimejipanga nje ya
bunge la nchi hiyo.
Libya iliandaa uchaguzi wa amani mwezi Julai mwaka huu, na wanasiasa wa nchi hiyo waliafikiana kuhusu jinsi ya kubuni serikali mpya siku ya Jumatano.

0 maoni:
Post a Comment