Viongozi wa Afrika Magharibi
wanatarajiwa kukutana katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja, kukamilisha mipango ya
kuwatuma wanajeshi kaskazini mwa Mali.
Mazungumzo hayo yatashughulika na
mapendekezo ya kutuma wanajeshi elfu kadha kuwaondoa wapiganaji wa Kiislamu,
iwapo juhudi za kufanya majadiliano hazitafanikiwa.
Baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa limewasihi viongozi Afrika magharibi kutayarisha mpango huo kufikia
mwisho wa mwezi huu.
Mataifa ya Magharibi yamejitolea
kutuma vikosi vya kutoa mafunzo kwa majeshi ya Afrika Magharibi.

0 maoni:
Post a Comment