Mkurugenzi mkuu wa shirika la BBC,
George Entwistle, amejiuzulu.
Amekuwa akishutumiwa kwa namna
alivyoshughulikia taarifa iliyopeperushwa katika kipindi cha Newsnight.
Taarifa hiyo kwa makosa ilimshutumu
aliyekuwa Waziri wa Fedha wakati wa serikali ya Conservative , Lord McAlpine,
kwamba alihusika katika kashfa ya kudhalilisha watoto.
Tayari shirika la BBC limekuwa
likichunguzwa vikali katika kashfa inayomhusu mtangazaji wake wa zamani Jimmy
Savile kwa madai ya kuwadhalilisha watoto.
Kipindi hicho cha Newsnight
kinadaiwa kuacha kwa makusudi kutangaza habari ya uchnguzi kuhusiana na kashfa
ya Bwana Savile.
Wakati wa kutangaza kujiuzulu
Jumamosi,usiku Bwana Entwistle alisema "ilikuwa ndilo jambo la heshima
kwangu kulifanya".
Akisimama kando yake Mwenyekiti wa
BBC Trust, Lord Patten alisema " huu ulikuwa moja wapo ya usiku wa majozi
katika maisha yangu ya umma".
"Muhimu kwa BBC ni jukumu lake
kama chombo cha habari kinachoaminika"
"Kama Mhariri Mkuu wa shirika
hili la habari, kwa heshima kubwa George amehiari kujiuzulu kutokana na makosa
yasiokubalika - uanahabari mbovu ambayo umezua malalamiko mengi".

0 maoni:
Post a Comment