Baraza la mawaziri nchini Kenya
linapendekeza mabadiliko makubwa kwa sheria za ndoa nchini humo .
Mswaada wawaliowasilisha
unapendekeza kuwa wanaume wanweza kuoa zaidi ya mke mmoja na hata kuharamisha
mahari ambapo familia ya mwanaume inalipa mahari hiyo.
Pia inataka kuhalalisha watu kuishi
pamoja kama mume na mke bila ya ndoa kwa kipindi cha miezi sita kama njia ya
kulinda watoto na wanwake wakati uhusiano huo unapovunjika.
Mapendekezo hayo tayari yamezua
hisia kali kutoka kwa jamii kwa ujumla. Aidha mswaada huo, lazima uidhinishwe
na bunge kabla ya kufanywa sheria.
Wengi wa wanaoishi maisha kama hayo
ni wanafunzi wa vyuo vikuu ambapo uhusianao kama huo unajulikana kama
"come we stay" au njoo tuishi pamoja kama mke na mume bila ya ndoa.
Wanafunzi hujipata katika uhusiano
kama huo kwa hata miaka minne au zaidi wakati wakisoma na punde baada ya
kuhitimu , huvunja uhusiano ule.
Mara nyingi watu huishi pamoja bila
ya kuoana kwa sababu za manufaa ya ule uhusiano
Wakati mwingine hata hupata watoto
wakati wa kipindi kile wanapoishi pamoja , na hapo ndipo mwanamue hutafuta njia
za kutoroka ili kukwepa majukumu yake.


0 maoni:
Post a Comment