Rais wa China Hu Jintao amefungua rasmi kongamano la
chama tawala ambalo linaanza mfumo mpya wa utawala ambapo watamchagua
kiongozi mara moja katika kipindi cha miaka kumi
Pia ametoa onyo kali kwa wafisadi akisema kuwa ufisadi bado unaendelea kuwa tatizo kubwa nchini humoAkihutubia zaidi ya wajumbe 2,000 mjini Beijing, bwana Hu alisema kuwa kukosa kushughulikia tatizo hilo, huenda kukasababisha pigo kubwa kwa chama.
Aidha Rais Hu anatazamiwa kujiuzulu kutoka wadhfa wake wa kiongozi wa chama na kumkabidhi Xi Ping anayeonekana kuwa kiongozi wa siku za usoni wa Uchina.
China ilipata mafanikio makubwa katika kipindi kilichopita ingawa changamaoto nazo zilikuwa nyingi.
Alitoa wito wa kuwepo malengo makubwa pamoja na kuhimiza bidii.
Hotuba yake ilifungua rasmi mkutano wa wiki moja utakaoshuhudia kuteuliwa kwa viongozi wapya wa chama.
Hali ya usalama imedhibitiwa mjini Beijing, huku wanaharakati wakiwa wamezuiliwa au kupewa kifungo cha nyumbani, kulingana na mashirika ya kibinadamu.


0 maoni:
Post a Comment