Meneja wa klabu ya soka ya
Arsenal ya Uingereza, Arsene Wenger, amemsifu sana Theo Walcott, kwa kuichezea
vizuri sana timu hiyo usiku wa Jumanne, katika mechi ambayo timu hiyo ilitoka
sare ya 2-2 katika mechi ya ugenini dhidi ya Schalke ya Ujerumani.
Lakini ilikuwa ni mara ya kwanza kucheza tangu mwanzo katika mechi ya Ulaya tangu mwezi Machi.
"Alicheza vizuri sana," alisema Wenger. "Alikuwa ni kati ya wachezaji wetu waliocheza vizuri sana."
Kulikuwa na wasiwasi kama Walcott angelicheza katika mechi ya jana, baada ya kuugua kwa muda, lakini kwa kutokuwepo Aaron Ramsey, ilibidia aingie uwanjani.



0 maoni:
Post a Comment