Meneja wa klabu ya soka ya
Manchester City ya Uingereza, Roberto Mancini, amesema hana matumaini tena ya
timu yake kufanya vyema katika mechi za klabu bingwa, baada ya Jumanne jioni,
ikiwa katika uwanja wa nyumbani, kutoka sare ya 2-2 ilipocheza na Ajax ya
Uholanzi.
"Kwa bahati mbaya tuliondoka tu na pointi moja, na nadhani hatuna tena matumaini ya kuendelea na ligi ya klabu bingwa," alisema Mancini.
Mancini, ambaye ni raia wa Italia, aligombana na waamuzi baada ya kipenga cha mwisho, kufuatia kuamini kwamba timu yake ilinyimwa ushindi.



0 maoni:
Post a Comment