Polisi mjini Cairo, Misri, wanasema wamegundua gengi la watu wanaouza
watoto ambalo linafikiriwa kuwa limeuza watoto wachanga 300.
Wauguzi wawili na daktari wa zahanati moja mjini Cairo ni
kati ya wale waliokamatwa, na polisi wanasema bado wanamsaka meneja wa zahanati
hiyo.
Inadaiwa kuwa wafanyakazi hao wa matibabu wamepasuwa waja
wazito wasiotaka kuzaa, na kuwatoa watoto wachanga ambao waliwauza kwa familia
zisokuwa na watoto.

0 maoni:
Post a Comment