MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

KILIMANJARO STARS USO KWA USO NA ZAMBIA
Siku chache tu, baada kumaliza katika nafasi ya nne kwenye mashindano ya CECAFA Senior Challenge Cup, Nchini Uganda, Timu taifa ya Tanzania iantarajiwa kurejea kambini kwa maandalizi ya mechi yao ya kirafiki dhidi ya mabingwa wa Afrika Zambia.
Kwa mujibu wa shirikisho la mchezo wa soka nchini Tanzania, Kilimanjaro Stars itavaana na Chipolopolo tarehe 22 mwezi huu katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
KIKOSI CHA KILIMANJARO STARS
 Kocha mkuu, Kim Poulsen tyari ametaja kikosi cha wachezaji 24 kitakachopiga kambi kujiandaa kwa mechi hiyo.
Aidha kwa mara ya kwanza kikosi hicho kinajumishwa wachezaji waliotia for a kwenye michuanp ya ligi kuu na pia michuana ya CECAFA.
Miongoni mwa wachezaji walioitwa kwa mara ya kwanza ni pamoja na Aishi Manul, Samih Nuhu, Issa Rashid na Mcha Khamis.
Sita kati yao ni miongoni mwa wachezaji walioakilisha Zanzibar katika michuano ya CECAFA iliyomalizika siku ya Jumamosi jijini Kampala, Uganda, ambapo Zanzibar ilimaliza katika nafasi ya tatu

Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment