KENYA YATOA SHERIA KALA KWA MADEREVA
Sheria mpya ya Kenya ya kuzuwia
madereva kuendesha magari kihatari, inaanza kutekelezwa Jumamosi.
Wakikutikana na makosa madereva
watakabili adhabu kali pamoja na kifungo cha maisha.
Madereva wa mabasi ya abiria, yaani
matatu, wamekuwa wakigoma tangu Alhamisi mjini Nairobi na kwengineko,
kulalamika juu ya sheria hiyo.
Wengi wanasema kuwa hawamudu faini
kubwa.
Lakini serikali imeazimia kupunguza
vifo mabara-barani.
Mwaka uliopita Wakenya zaidi ya
3,000 wamekufa kwenye ajali za barabarani.

0 maoni:
Post a Comment