OSCAR PISORIUS KUKATA TAMAA
Mwanariadha wa Afrika Kusini, Oscar
Pistorius, anayetuhumiwa kwa mauaji ya mpenzi wake, huenda akajinyonga, rafiki
wa karibu wa familia yake ameambia BBC.
Mwanariadha huyo, amejipata pabaya
baada ya kulazimika kuuza baadhi ya mali zake ili kugharamia kesi yake, alisema
Mike Azzie.
Bwana Azzie alitoa matamshi yake
katika kipindi cha BBC, kuhusu kesi inayomkabili Pistorius, ambapo mwanariadha
huyo anakanusha madai hayo.
Wakati huouo, mawakili wa
mwanariadha huyo , wameomba mahakama kulegeza vikwazo vya dhamana aliyopewa.
Bwana Pistorius, ambaye anakabiliwa
na kesi kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp nyumbani kwake mwezi jana,
anakanusha madai kuwa alipanga kumuua Reeva akisema hakujua kama ni yeye wakati
wa kitendo hicho.
Aliachiliwa kwa dhamana tarehe 22
mwezi Februari na kesi itasikilizwa tena mwezi Juni.
Bwana Azzie, ambaye amekuwa
akiwasiliana na Pistorius, alisema kuwa ana wasiwasi kuhusu hali yake ya
kiakili
Azzie, ambaye Oscar humuiya mjomba,
Mike, alisema kuwa manariadha huyo, amelazimika kuuza farasi wake ili kugharamia
kesi yake.
''Hajiamini hata kidogo na ni kama
tu ambaye anazunguka zunguka asijue anakokwenda,'' alisema bwana Azzie
"naweza kusema kwa kuongea naye
tu, anaonekana kama mtu aliyevunjika moyo sana. Naweza kusema anakaa kama mtu
ambaye amekata tamaa na hata anaweza kujinyonga . Na hiyo inatia wasiwasi
mkubwa,'' alisema Azzie katika kipindi maalum kuhusu Oscar.
0 maoni:
Post a Comment