BIA ya Safari Lager inayotengenezwa na kampuni ya bia ya
Tanzania (TBL) imenyakua tuzo ya ubingwa wa jumla katika mashindano ya kwanza
ya ubora wa bia yaliyoandaliwa na taasisi ya The Institute of Brewing and
Distilling (IBD).
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam
jana Meneja wa bia hiyo Oscar Shelukindo, alisema mashindano hayo yalifanyika
kuanzia Machi tatu had inane mwaka huu katika jiji la Accra Ghana.
Alisema katika mashindano hayo yalishuhudia kampuni ya
kutengeneza bia ya SABMiller Afrika ikipokea tuzo 10 kati ya 13 zilizotolewa
ikiwamo tuzo hiyo ya ubingwa wa jumla.
“Bia ya Safari Lager inafahamika vizuri kwa ladha yake
yenye ubora wa hali ya juu usiobadilika hili si jambo geni miongoni mwa
Watanzania, lakini kutunikiwa tuzo ya ubingwa wa jumla katika mashindano
yanayoshirikisha bia nyingi za bara la Afrika ni jambo la kutia for asana.
“Pamoja na hilo bia ya Safari Lager pia imenyakua tuzo ya
ubora wa bia za Afrika zenye kiwango cha kilevi cha zaidi ya asilimia tano, hii
inadhihirisha kwamba tumejizatiti katika umakini wa utengenezaji wa bia hii.
“Tuzo hii ya ubingwa wa jumla inawapa wateja wetu uhakika
kwamba kweli wanakunywa bia bingwa,” alisema.
Alisema katika mashindano hayo zaidi ya bia 50 kutoka katika
makampuni maarufu yanayotengeneza bia Afrika yalishiriki mashindano hayo
yakiwamo makampuni kama SABMiller Afrika na SAB Ltd.
Aidha alisema katika mashindano hayo taasisi hiyo ya IB
ilikusanya watalaam huru kutoka katika mabara matatu tofauti ili kuonja bia na
kuto maamuzi yasiyo na upendelea wowote.
“Katika mashindano haya bia hizi zilipimwa katika makundi
tofauti kama vile bia zinazotengenzwa kwa kutumia malighafi zinazopatikana
sehemu inapotengenezwa bia yenyewe, bia zeny kiwango cha kilevi chini ya
asilimia tano, na pia kundi la bia zenye kiwango cha kilevi cha zaidi ya
asilimi tani,” Alisema.
0 maoni:
Post a Comment