ABU QATADA
KUBAKI UINGEREZA
Serikali ya Uingereza hatimaye
imeshindwa katika dakika za mwisho kwenye kesi ya kumuondosha nchini hapa
mhubiri wa dini ya kiislamu mwenye itikadi kali Abu Qatada kwenda nchini
Jordan.
Abu Qatada amekuwa akitakiwa na
serikali ya Jordan baada ya kupatikana na hatia ya makosa ya ugaidi mwaka 1999.
Serikali ya Uingereza,imekuwa
ikijaribu kumuondoa nchini Uingereza,kiongozi huyo ambaye ni mhubiri wa dini ya
kiislamu kwa zaidi ya miaka kumi iliyopita bila mafanikio,baada ya mabishano
makubwa ya kisheria.
Hili limekuwa ni anguko jingine kwa
Serikali ya Uingereza hasa wizara ya mambo ya ndani, ambapo Mhubiri huyo wa
dini ya Kiislamu anayetambulika kisheria kama Omary Mohammed Othman,maarufu
kama Abu Qatada,ameendelea kupata kinga ya mahakama ya kusalia nchini
Uingereza.
Mahakama ya rufaa mjini London,kwa pamoja
imeyakataa maombi ya Waziri wa mambo ya ndani Theresa May,ambaye alipeleka kesi
kwa niaba ya Serikali

0 maoni:
Post a Comment