MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG
TIGO NA ZARA KUZINDUA NUSU MARATNON
KAMPUNI ya ZARA Tanzania Adventure kwa kushirikiana na kampuni ya simu za mikononi ya Tigo, zimezindua mashindano ya nusu marathon zijulikanazo kama ‘Ngorongoro Half Marathon’ zinazotarajiwa kufanyika Aprili 6 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi huo Mratibu wa mashindano hayo Datus Joseph kutoka Zara alisema mashindano hayo yatafanyika katika mji mdogo wa Karatu mkoani Arusha.
Alisema mbio hizo kwa mwaka huu yamebeba ujumbe wa ‘Mbio za Mapambano dhidi ya Malaria’
“Mnamo mwaka 2010, kampuni ya  Zara Tanzania adventures ilianzisha na kuwa mdhamini mkuu wa  mbio za watoto za kilomita tano zilipewa jina la ‘Ngorongoro Run: Kids’ Fun Run’, mbio ambazo zimetia chachu zaidi mbio hizo za Ngorongoro Marathon.
“Zaidi ya wakazi  5,000 wa Karatu wanashiriki na kuzifurahia sana mbio hizo ambapo pia hupata fursa ya kujifunza masuala mbalimbali ya mapambano dhidi ya malaria.
 “Mbio za Ngorongoro Marathon mwaka huu ni za kipekee sana kwani zinajumuisha ushindanishaji wa makampuni mbalimbali ulioandaliwa na kampuni ya mtandao wa simu za mkononi Tigo  yatakayofanyika kabla ya kuanza kwa mashindano hayo ambapo mshindi ataibuka na kitita cha dola za kimarekani  20,000 ambazo atajitolea kwa taasisi yeyote yenye uhitaji atakayoichagua.
Alisema katika ufunguzi wa mbio hizo unatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya watu  3000 ambapo huku Naibu waziri wa Mali asili na Utalii Lazaro Nyalandu akitarajiwa kufunga mbio hizo.
Kwa upande wake Meneja chapa wa kampuni ya Tigo alisema kampuni hiyo imeamua kushiriki kuandaa mbio hizo ili kuwaelimisha wananchi namna ya kupambana na malaria.

Alisema pia mashindano hayo ni kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia jamii kupambana na malaria, kuboresha huduma za hosptali pamoja na huduma ya mama na mtoto.
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment