YANGA YATOA TAMKO
Klabu ya Yanga SC , miongoni mwa klabu kongwe ya mpira hapa nchini Tanzania , imetoa taarifa ya kuzuiya matumizi ya nembo ya klabu hiyo kinyume na sheria.
Taarifa hiyo imetolewa kama tahadhari na angalizo kuwa nembo ya Yanga ni nembo iliyosajiliwa rasmi kwa msajili wa TRADEMARKS na kumilikiwa na klabu ya Yanga tu, nembo hiyo ilisajiliwa june 4, 2009,
Tamko hilo limetokana na makampuni na wafanya biashara wakubwa mbalimbali kutumia nembo hiyo katika bidhaa zao na kutumia nembo hiyo, hivyo klabu ya Yanga imeonya vikali matumizi ya nembo hiyo kinyume cha sheria, kwa yoyote yule au kampuni yoyote itakayo tumia nembo hiyo sheria kali zitachukuliwa dhidi yao.
Yanga imetoa ushauri kwa wale wanaotaka kuleta bidhaa zenye nembo ya Yanga, wanatakiwa kufanya mawasiliano na klabu hiyo ili waweze kufanya hivyo, kinyume na hivyo hatua kali dhidi yao zitachukuliwa.

0 maoni:
Post a Comment