Mchezaji wa kikosi cha wekundu wa msimbazi, Amri
Kiemba, amesaini mkataba mpya ambao umegharimu kiasi cha milioni 35, na
kumfanya asalie kwenye kikosi hicho.
Mchana wa leo Simba ilikuwa kwenye
jitihada nzito kuhakikisha inamzuia Kiemba kusaini Yanga kwa kumpa ofa nono ya
mkataba mpya, Kiemba alikuwa akihitaji kiasi cha millioni 38 ili asaini
msimbazi lakini baada ya mazungumzo marefu Kiemba amekubali kusaini kwa kiasi
cha millioni 35 kwa miaka miwili hijayo katika kikosi hicho.
Mchezaji huyo atakuwa anapokea
kitita cha milioni mbili kila mwenzi kwa kipindi hicho cha miaka miwili
kilabuni hapo, mkataba wake ulisainiwa mbele ya kaimu makamu mwenyekiti Mzee
Kinesi.
0 maoni:
Post a Comment