
Siku mbili baada ya
Rais wa Sudan kuiomba Marekani kumpa Visa ya kusafiri nchini humo kuhudhuria
mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, wito umetolewa kwa
taifa hilo kumkamata Bashir na kumkamabidhi kwa mahakama ya ICC.
Mkutano huo utafanyika
wiki ijayo.
Ombi hilo limetolewa
na ICC kwa Marekani na kuitaka impe Visa Bashir na kisha kumkamata na
kumkabidhi kwa mahakama hiyo pindi tu atakapotua nchini humo.
Bashir anatakikana na
mahakama ya ICC kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya binadamu na pia kuamuru mauaji
ya halaiki katika jimbo la Darfur.
Marekani ilisema kuwa
ilipokea ombi la Bashir kutaka Visa na kulitaja ombi hilo kama la kuudhi na
kejeli kubwa kwa taifa hilo. Ilimtaka Bashir kwanza kujikabidhi kwa mahakamya
ICC kabla ya kutaka kuingia Marekani.
Hata hivyo Marekani
sio mwanachama wa mahakama ya ICC na kwa hivyo , kisheria sio lazima itimize
matakwa ya mahakama hiyo juu ya Bashir.
Marekani imekuwa
katika msitari wa mbele kutaka Bashir akamatwe kwa madai ya uhalifu dhidi yake
ili akabiliwa na sheria za kimataifa
Shirika la habari la
Reuters lilisema kua mahakama imeshauri Marekani kumkamata Bashir na kumkabidhi
kwa ICC ikiwa ataingia nchini humo.
Vibali viwili vya
kumkamata Bashir vilitolewa mwaka 2009 na 2010 kwa madai ya uhalifu dhidi ya
binadamu.
Hata hivyo Sudan
imepuuza hatua ya ICC kumtaka Bashir kwa makosa ya Darfur wakisema kuwa madai
hayo yameongezwa chumvi, na nchi hiyo imekataa kuitambua mahakama hiyo ikisema
kuwa ni sehemu ya njama ya nchi za magharibi dhidi ya Afrika
Kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment