![]() |
Ni siku moja tu tokea kutangazwa kuwa Dogo janja amefukuzwa katika kundi la Watanashati chini ya Ostazi Juma na Musoma, kutokana na sababu za utovu wa nidhamu lakini leo hii Ostaz, ameamua kumrudisha tena kundini Dogo Janja.
Inasemekana kuwa dongo janja, amekubali makosa na kumuakikishia kuwa amebadilika “ nimeamua kumrudisha kwa sababu yale mambo yaliopelekea mpaka mimi kutoa maamuzi yale niliyoyatoa jana, yani kawa kama mtu mzima mwenyewe akili timamu, na mtu yeyote anayefikiria na akaona kwamba hili ni kosa akasema kwamba ntajirudi, ni kumpa nafasi ya kumsikiliza.
Kwa hiyo jana tulikaa kkikao cha familia nyumbani kwangu, tukazungumza na ni kweli ameona kwamba ni bora aache baadhi ya mambo ambayo hayakuwa mazuri kwenye jamii,, na mimi ninachokitaka Dogo Janja, awe mtu bora , awe mzuri katika jamii Na yeye ameniahiji kwamba, atawahakikishia Watanzania kwamba atakuwa Dogo Janja ambaye Watanzania wanamtaka wao. Haya yalikuwa maneno ya Ostazi juma mara baada ya kufanyiwa mahojiano na mtandao wa Times Fm.
|
MWERA AMAZING BLOG
- Blogger Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

0 maoni:
Post a Comment