Maujia ya tembo yameongezeka nchini Tanzania tangia serikali ya nchi hiyo kusitisha Opereshieni tokomeza kutokana na kuwepo madai kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa haki za binadamu
Naibu waziri wa Maliasili na utalii nchini Tanzania Lazaro Nyarandu amesema kuwa idadi ya tembo 60 wameuawa katika kipindi cha miezi miwili tu ya mwezi Novemba na Disemba ikilinganishwa na tembo wawili tu waliouawa mwezi wa kumi mwaka huu
Hata hivyo idara za ulinzi zilikubaliana kuwaua majangili watakaobainika wakiwaua tembo hao kipindi ambacho msako huo ulikuwa ukiendelea mwezi Oktoba mwaka huu
Hata hivyo serikali ilisitisha operesheni hiyo kufuatia malalamiko kwamba watekelezaji wa msako huo walikuwa wakikiuka haki za binadamu
Waziri mkuu wa Tanzania alikaririwa akisema operesheni hiyo ilikuwa na nia njema lakini taarifa za kuwepo vitendo vya mauajia na ukikwaji wa haki za binadamu ndicho ambacho hakikubaliki na serikali
0 maoni:
Post a Comment