Maafisa
sita wa shirikisho la soka duniani Fifa wamekamatwa katika hoteli moja mjini
Zurich,Switzerland. kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa...........
Watuhuhumiwa
hao ambao wanasemekana kuwa ni pamoja na makamu wa rais wa Fifa,wanashikiliwa
wakisubiri kusafirishwa kwenda Marekani.
Shutma
hizo zinahusisha rushwa ya takriban kiasi cha dola za Marekani milioni 100 kwa
kipindi cha zaidi ya miaka 20
Wanachama
wa Fifa wanakutana mjini Zurich kwa ajili ya mkutano wao wa mwaka siku ya
ijumaa, ambapo rais wa Shirikisho hilo Sepp Blatter anawania muhula wa tano.
Mwana
mfalme Ali Bin Al-Hussein wa Jordan,ambaye ndiye mpinzani pekee wa Blatter
amesema tukio hilo ni "baya kwa maendeleo ya soka".
Gazeti
la New York Times limesema askari kanzu walichukua funguo za chumba cha hoteli
kutoka eneo la mapokezi ya hoteli ya Baur au Lac hotel ambayo maafisa hao
walikuwa wakiishi na kuingia vyumbani mwao.Gazeti hilo limesema Operesheni hiyo
ilifanyika kwa utulivu.
Jeffrey
Webb, Mkuu wa shirikisho la Amerika ya Kaskazini na Kati na Visiwa vya
Caribbean ametajwa kuwa mmoja kati ya maafisa waliokamatwa.
Maafisa
wengine wa Fifa walishuhudiwa na BBC wakisindikizwa na Polisi kutoka kwenye
hoteli hiyo ni:
Mkuu
wa Shirikisho la soka la Costa Rica, Erduado Li, ambaye alikuwa akitarajia
kuwepo kwenye mkutano wa kamati ya Fifa siku ya ijumaa.Wengine ni rais wa
shirikisho la Uruguay Eugenio Figueredo,rais wa shirikisho la soka Amerika
kusini Conmebol na wa Brazil,Jose Maria Marin,mwanakamati ndani ya Fifa,Polisi
walionekana wamebeba mikoba yake kwenye mifuko ya Plastiki.
Watu
wengi wamekuwa wakijiuliza ni kwa vipi Blatter amekuwa Kiongozi wa Fifa kwa
muda mrefu, pamoja na kuwepo kwa ripoti nyingi za vitendo vya rushwa lakini
ameendelea kushikilia wadhifa huo.
Wizara
ya sheria ya Uswiss imesema katika tamko lake siku ya jumatano kuwa maafisa wa
serikali ya Marekani waliwashuku maafisa hao kupokea rushwa ya dola milioni
100, tangu mwanzoni mwa miaka ya 1990 kwa ajili ya michuano ya Amerika ya kati.
Serikali
ya Uswiss imesema itaidhinisha haraka kusafirishwa kwao.
Mwanzoni
mwa mwezi huu, Blatter alisema anafahamu baadhi ya wafanyakazi wenzake wa
zamani walikuwa wakichunguzwa lakini amekanusha kuwa uchunguzi huo ulimhusu pia
Kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment