Mshambuliaji wa Nigeria na timu ya Wanawake ya
Liverpool, Asisat Oshoala ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya BBC ya mwanasoka
bora wa mwaka............
Oshoala,
mwenye umri wa miaka 20 ni mchezaji wa kwanza kushinda tuzo mpya kutoka BBC
World Service,kwa kura zilizopigwa na wapenzi wa kandanda duniani.
Mwanadada
huyu amemuangusha Veronica Boquete wa Uhispania na Nadine Kessler wa
Ujerumani,Scot Kim Little na Marta wa Brazil.
"ninapenda
kutoa shukrani zangu kwa BBC,mashabiki wangu duniani na kila mmoja aliyepiga
kura" alisema.
Tuzo
hii ni ya kwanza kufanyika na Shirika la utangazaji la kimataifa.
Oshoala,
ambaye ni mchezaji mwenye umri mdogo kuliko wote kati ya wapinzani wake,
alikuwa mfungaji bora na alipigiwa kura wakati wa michuano ya kombe la dunia la
wachezaji wa umri wa chini ya miaka 20 nchini Canada kipindi cha majira ya joto
kilichopita.
Jitihada
zake ziliifikisha Nigeria katika hatua ya Fainali ambapo ilikutana na
Ujerumani, ambapo Ujerumani ilipata ushindi mwembamba dhidi ya Nigeria.
Pia
alitoa mchango mkubwa katika timu ya wanawake ya Nigeria katika kutwaa ushindi
wa kombe la mabingwa Afrika kwa wanawake mwezi Oktoba.
Hatua
hiyo imeiwezesha Nigeria kufuzu kushiriki michuano ya kombe la dunia kwa
wanawake nchini Canada inayoanza tarehe 6 mwezi Juni
Kutoka BBC Swahili.
0 maoni:
Post a Comment