MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

UINGEREZA ,UFARANSA KUWAKABILI WAHAMIAJI

Kampuni wa usafiri inayofanya safari zake kati ya Ufaransa na Uingereza ya Eurotunnel imesema maelfu ya wahamiaji wamekuwa wakijaribu kuingia nchini Uingereza kupitia usafiri huo...........


Ripoti ya kampuni hiyo imebainisha kuwa idadi ya majaribio ya wahamiaji kutaka kuvuka mpaka kupitia usafiri aina hiyo ya usafiri imeongezeka mno,kwani wahamiaji hao watu hao wanajificha kwenye magari ya mizigo,kupanda vizuizi ilimradi tu waingine katika vyombo hivyo vya usafiri na kuvuka.

Katika mkutano wa Mawaziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa na Uingereza uliofanyika mjini London,mbinu za pamoja kuweza kudhibiti wahamiaji hao kuvuka zimejadiliwa na kuelezea hali kuwa ni tatizo kubwa kwa sasa.

Wahamiaji hao kutoka nchi za Sudani na Afghanstan waliopo bandari ya Calais nchini ufaransa ya Calais ndiyo waliobainika kutaka kuvuka kwenda nchini Uingereza kwa mfumo huo, wengi wa wahamiaji hao wanatoka nchini Sudan na Afghanstan.

Mwaziri hao wa mambo ya ndani wa Ufaransa na Uingereza wanasema wamebaliana tutafanya kazi pamoja kuwarejesha wahamiaji hawa ambao wengi wao wanatoka Afrika Magharibi,na kuwahakikishia watu kwamba safari za aina hii haziwi lango kuu la wahamiaji kuingia Uingereza.


Na tayari serikali ya Ufaransa imekwisha anza kuweza jitihada za ziada kama idadi zaidi ya askari,na uingereza itatoa kiasi cha paundi million saba kuimarisha ulinzi,japo kuwa Mbunge wa Bunge la Ulaya Claude Moraes anasema haamini kama hatua ya kuwarejesha wahamiaji hao makwao kutasaidia kutatua tatizo hilo
chanzo BBC
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment