H. KIMATAIFA Watoto watano wa Tanzania wenye
ulemavu wa ngozi waliokuwa wamekatwa viungo vya miili yao wamewekewa mikono na
miguu ya bandia katika hospitali iliyopo nchini Marekani..............
Watoto
hawa ni miongoni mwa mamia ya watu wanye ulemavu wa ngozi nchini humo ambao
wamekuwa wakiwindwa na watu wanaotaka viungo vya miili yao kwa shughuli za
kishirikina
Watoto
hao, mmoja wa kike na wanne wa kiume kutoka mikoa ya Kaskazini Magharibi na
Kusini Magharibi mwa Tanzania, wamekuwa wakipokea matibabu hayo katika
hospitali ya watoto Philadelphia Shriners Hospital iliyopo jijini New York.
Wakiwa
na umri kati ya miaka 6 hadi 18, wanne wa watoto hawa walipatwa na majeraha
makubwa ya kukatwa mikono na miguu yao, huku mmoja wao akiwa amekatwa taya na
meno.
Tayari
watoto wanne wamekwisha wekewa mikono na miguu ya bandia, wakati yule
aliyekatwa taya akitarajiwa matibabu yake kuchukua muda mrefu zaidi
Shirika
la msaada la Kimarekani Global Medical Relief Fund linafadhili matibabu ya
watoto hawa.
Ofisa
kutoka shirika la Under the Same Sun Martin Haule anasema watoto wanaendelea
vizuri na kwamba ni wenye furaha
Ameiambia
BBC kwamba wanatarajiwa kurudi nyumbani Tanzania mnamo mwezi Septemba
Kwa
mujibu wa Umoja wa Mataifa, ulemavu wa ngozi unaathiri takribani mtu mmoja
katika kila watu 15,000 nchini Tanzania.
Watu
hawa wanawindwa kwa ajili ya viungo vyao, ambavyo vinatakiwa katika biashara
haramu kwa matumizi ya shughuri za kishirikina
.
0 maoni:
Post a Comment