JE WAJUA ? Kidimbwi cha kuogelea chenye urefu
wa mita 25 kinachounganisha kilele cha majumba mawili marefu yenye ghorofa 10
kitajengwa mjini London...........
Kidimbwi
hicho kinachoitwa ''Sky Pool'' ni cha kwanza duniani na kitakuwa na eneo la
chini lililo wazi.Uwazi huo utawasaidia waogoleaji kuwaona raia wanaotembea
chini ya majumba hayo kwa urefu wa mita 35.
Kampuni
ya Eckersley O'Callaghan ambayo imeshirikiana na ile ya Apple kuhusu mtindo wa
kidimbwi hicho cha kuogelea itatengeza mradi huo.
Kidimbwi
hicho ni miongoni mwa miradi ya ujenzi ya maeneo ya kujivinjari kwa jina
Embassy Gardens at Nine Elms,karibu na kituo cha umeme cha Battersea
Inatarajiwa
kuwa mradi huo utakamilika ifikiapo mwaka 2019,lakini mtindo huo una changamoto
zake hususan kutokana na hatua kwamba kidimbwi hicho kitazuiliwa na misukumo
itakayotoka kutoka kuta za majumba hayo mawili ambayo yamejengwa na misingi
tofauti.
''Upepo
unapovuma majumba hayo huyumba tofauti na hivyobasi kuwa changamoto kwa
watengezaji wa kidimbwi hicho'' kulingana na Brian Eckersley
0 maoni:
Post a Comment