H.KIMATAIFA Kiongozi mkuu wa jeshi la muungano
wa Afrika linalohudumu nchini Somalia, anasema kuwa wanajeshi watatu wa kikosi
hicho wameshtakiwa kuhusiana na mauaji ya mwezi uliopita ya kundi moja la raia...............
Maman
Sidikou aliomba msamaha na akatoa kile ambacho amesema ni rambirambi kwa jamaa
ya watu saba wa familia moja waliopigwa risasi katika mji wa Merka, kusini mwa
mji mkuu Mogadishu.
Kwa
mjibu wa kundi moja la kutetea haki za binaadamu- Human Rights Watch, wanajeshi
wa umoja wa Afrika kutoka Uganda waliwashambulia kwa risasi watu waliokuwa
wakihudhuria harusi baada ya msafara wao kulipuliwa kwa bomu.
Askari
hao watahukumiwa katika mahakama ya kijeshi.
Chanzo BBC Swahili.
0 maoni:
Post a Comment