HABARI Mtu wa kwanza kabisa kuhukumiwa na
mahakama ya kimataifa ya makosa ya Jinai iliyoko the Hague nchini Uholanzi,
ameiambia mahakam hiyo kuwa anataka kurejea nyumbani ili kusomea chanzo cha
mapigano ya kikabila...............
Mbabe
huyo wa kivita raia wa Congo, Thomas Lubanga, alisema hayo wakati wa kusikizwa
kwa kesi yake, ambapo majaji wanajaribu kuona iwapo anaweza
kufunguliwa mapema
baada ya kuhudumia robo tatu ya kifungo chake.
Ameiambia
mahakama hiyo ya ICC kuwa, amegundua uwezo wake mkubwa alio nao wa kuleta
uwelewano na upatanishi nchini DRC.
Bwana
Lubanga anahudumia jela miaka kumi na nne kwa kuwatumia watoto kama wanajeshi
katika vita na makosa mengine.
Amekuwa kifungoni tangu mwaka 2006.
Chanzo BBC Swahili.
0 maoni:
Post a Comment