Waziri Mkuu wa
Uingereza David Cameron anatarajiwa kutangaza mipango hapo baadae ya kuongeza
idadi ya Wakimbizi kuingia nchini humo.
Hakuna idadi kamili
iliyoafikiwa, lakini Cameron alisema Uingereza itaendelea kuwachukua maelfu.
Wakimbizi wengine
wanatarajiwa kutoka kwenye Makambi ya Umoja wa Mataifa katika mpaka wa Syria,
na si miongoni mwa wale ambao tayari wako Ulaya.
Waziri Mkuu,ambaye
amepata shinikizo kuongeza nguvu kushughulikia tatizo la wahamiaji, atatoa
kauli yake nchini Uhispania baada ya mazungumzo na Viongozi wenzao.
Cameron anakutana na
wenzake wa Portugal na Uhispania kwa ajili ya mazungumzo ambayo yametawaliwa
zaidi na maswala ya mzozo wa uhamiaji.
Chanzo BBC Swahili.
0 maoni:
Post a Comment