Mwelekezi wa video mpya
ya Taylor Swift iliyoshutumiwa kwa kuonyesha picha mbaya ya Afrika amejitokeza
na kuitetea vikali.
Video hiyo ya wimbo
Wildest Dreams imedaiwa kuendeleza dhana potovu ya maisha bora iliyokuwa na
wakoloni barani Afrika.
Lakini mwelekezi Joseph
Kahn amesema "video hiyo haihusu ukoloni bali ni simulizi ya kisa cha
mapenzi katika kundi la waandalizi filamu Afrika, 1950".
Swift hajazungumzia
utata uliogubika video hiyo.
Kupitia taarifa, Kahn
amekanusha madai kwamba video hiyo imeshirikisha Wazungu pekee.
“Ukweli ni kwamba sio
tu kuwa kuna watu wa asili nyingine kwenye video hiyo, bali pia wabunifu
waliofanyia kazi video hiyo ni wa asili nyingine.”
Ameeleza kuwa yeye ni
wa asili ya Asia na Amerika, naye produsa wa video hiyo Jill Hardin na mhariri
Chancler Haynes ni Waafrika Waamerika.
“Tuliamua kwa pamoja
kwamba haingekuwa sahihi kihistoria kujaza waigizaji weusi kwenye video hiyo
kwani tungeshutumiwa na kudaiwa kujaribu kuandika upya historia.
“Video hii inaonyesha
mambo ya zamani kupitia watu wanaoishi kwa sasa na tunajivunia kazi yetu.”
"Kuna Waafrika
weusi kwenye video hiyo, lakini sikuangazia sana watu wengine kwani muda mwingi
unachukuliwa na Taylor na Scott (Eastwood).''
Video hiyo imetazamwa
mara milioni 19 tangu ipakiwe mtandaoni Jumatatu.
kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment