Katika hotuba yake
iliyojaa kila aina ya hisia kali, Rais Obama amebainisha wazi mipango yake juu
ya kuweka mikakati thabiti ya udhibiti silaha za moto, akisema kwamba Marekani
haipaswi kukubali mauaji kama gharama ya uhuru.
Obama amesema kwamba
hatua madhubuti zinapaswa kuchukuliwa ambazo zitajumuisha ufuatiliaji wa tangu
awali wa upatikanaji silaha, pia uchunguzi wa afya ya akili utazingatiwa na hii
ni pamoja na kumbukumbu za uhalifu wa mtuhumiwa zitahusishwa pia.
Pamoja na machozi
yaliyokuwa yanashuka njia mbili juu ya mashavu ya Rais Barack Obama, amesema
suala la upatikanaji wa silaha lilikuwa limeliteka nyara bunge la Congress,
lakini suala hilo halitaiteka nyara Marekani yote wakati huu ambapo uhalifu wa
silaha umeua wamarekani wengi mno ukilinganisha na ajali za barabarani.
Rais Obama anatarajiwa
kuweka hadharani hatua zitakazochukuliwa dhidi ya matumizi mabaya ya silaha na
hasa ikizingatiwa hii ni miaka ya upinzani mkali katika serikali yake.
Lakini chama cha wauza
silaha nchini Marekani kilichoundwa mnamo mwaka 1871, chenye kufuatilia
matumizi salama ya silaha na usalama wa silaha nchini Marekani na pia hutetea
haki ya kuwa na silaha ama kuibeba wamekosoa hotuba ya Rais na kusema kwamba
mapendekezo yake hayatazuia mauaji ya halaiki kutokana na aliyoyasema katika
hotuba yake.
KUTOKA BBCSwahili.
0 maoni:
Post a Comment