
Umoja wa Ulaya na viongozi
wa Uturuki waliokutana mjini Brussels wameshindwa kufikia muafaka wa suluhisho
la mgogoro wa wahamiaji.
Uturuki inatuhumiwa na
Jumuiya ya Ulaya kuwa na wimbi kubwa la wahamiaji wanaovuka ,na kuchukua msaada
unaozidi euro bilioni tatu.
kutokana na hali hiyo
Umoja wa ulaya umeitaka Uturuki kuwachukua wahamiaji ambao hawakukidhi vigezo
vya kupata hifadhi na kuongeza jitihada zaidi za kuwazuia kuvuka bahari ya
Aegean kuelekea Ugiriki.
Raisi wa bunge la Ulaya
,Martin Schulz amesema suala la maombi ya uturuki kutaka kuongezewa euro
bilioni tatu ili kulipia huduma za afya na shule kwa ajili ya wakimbizi
wanaokaa nje ya kambi bado linajadiliwa katika mkutano huo wa nchi za umoja wa
ulaya.
Hata hivyo Katibu mkuu
wa NATO amesema mkutano huo ulioanza jana unafahamika wazi malengo yake katika
nchi ya Uturuki na ukanda wa bahari ulioko upande wa ugiriki. Ameyasema wakati
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari,Jens Stoltenberg na Waziri
Mkuu wa Uturuki Jens Stoltenberg.
Kutoka BBC Swahili
0 maoni:
Post a Comment