Rais wa Marekani Barack Obama amemwambia Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan kuwa nchi ya Marekani ipo pamoja na watu wa Uturuki katika wakati huu mgumu baada ya kushambuliwa kwa uwanja wake wa ndege wa Istanbul kwa mabomu ya kujitoa muhanga siku ya Jumanne.
Maafisa nchini Uturuki wanaamini kuwa wanamgmbo wa IS walihusika katika shambulizi hilo lililouwa zaidi ya watu 40 na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa.
Obama anasema kuwa amempigia simu Rais wa Uturuki kumpa salam za rambirambi sambamba na kusisitiza dhamira ya nchi yake kuendeleza mapigano dhidi ya IS.
Shambulio hilo linatajwa kuwa limeuwa watu wengi zaidi nchini humo ikilinganishwa na mashambulizi kadhaa yaliyopita.
kutoka BBC Swahili
0 maoni:
Post a Comment