Kufuatia Uingereza kujitoa ndani ya Jumuiya ya Ulaya mijadala na kauli zinaendelea kutolewa kutathimini matokeo yake katika Nyanja tofauti ambapo Marekani imeleezea mtazamo mpya kidplomasia nani ya Ulaya.
Balozi wa NATO wa zamani kutoka Marekani, Nicholas Burns,amesema kujitoa kwa Uingereza katika jumuiya ya Ulaya kunatarajiwa kubadili uelekeo wa Marekani na kuifanya Ujerumani kuwa kitovu kipya cha masuala ya kidplomasia ndani ya Ulaya.
Nafikiri Ujerumani imekuwa imekuwa ikiimarika ndani ya Ulaya kwa muda mrefu sasa.
Hivyo kama Uingereza ikijiondoa EU tutapata mshirika mpya ,Ujerumani,na haitakuwa kwamba na ubora wa ushirikiano kama wa Uingereza tu,bali tutakuwa tumepata mshirika makini zaidi ambaye ni Ujerumani.’’
Burns amesema Uingereza ilikuwa ikiiwakilisha Marekani ndani ya jumuiya ya Ulaya,hivyo
Wamarekani kuna wakati wana sahau kama Jumuiya ya Ulaya ni mdau wetu mkubwa kibiashara,mwekezaji wetu mkubwa, na Ulaya ni mkusanyiko wa asasi za kimarekani duniani na ndani ya NATO.
Hivyo uingereza ni mwanachama muhimu ndani ya asasi hizo za Marekani.
Nafikiri wanasiasa wa Marekani wana wajibu wa kuishawishi Uingereza kusalia EU.
Kutoka BBC Swahili
0 maoni:
Post a Comment