
Waziri wa fedha wa Afrika Kusini,
Pravin Gordhan, amegomea mwito wa polisi nchini humo waliomtaka kuripoti
kituo cha polisi, na kusema kwamba tuhuma dhidi yake hazina msingi.
Vyombo vya habari nchini Afrika Kusini zinaeleza kuwa sababu ya mwito huo zinatokana na uchunguzi uliofanywa dhidi ya kitengo alichowahi kukisimamaia cha masuala ya kodi ambacho kinashutumiwa kwa kuwachunguza wanasiasa nchini humo.
Upande wa upinzani unahisi kuwa waziri huyo ni mwathirika wa jaribio la kumdhoofisha linalofanywa na wafuasi wa Rais Jacob Zuma.
Kutoka BBC Swahili.
0 maoni:
Post a Comment