MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

Beki wa Arsenal Kieran Gibbs kwenda West Brom

Kieran GibbsHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKieran Gibbs alicheza mechi 11 Ligi ya Premia msimu uliopita
West Brom wanakaribia kukamilisha ununuzi wa beki wa kushoto wa Arsenal Kieran Gibbs.
Klabu hizo mbili zimeafikiana ada ya £5m kwa mchezaji huyo wa miaka 27 ambaye pia alikuwa akifanya mashauriano na Watford pamoja na klabu ya Galatasaray ya uturuki.
Gibbs bado atahitajika kufanyiwa uchunguzi wa matibabu kabla ya kutia saini mkataba wake.
Kwingineko, Arsenal wamejiunga na Manchester City na Leicester City katika kutaka kumsajili beki wa kati wa West Brom Jonny Evans.
Evans ataruhusiwa kuondoka Hawthorns iwapo tu West brom watafanikiwa kupata mchezaji wa kujaza pengo atakaloacha.


    Wanamtaka zaidi mchezaji wa Manchester City Eliaquim Mangala na iwapo Manchester City watamtaka kwa kweli Evans, basi uhamisho huo utakuwa rahisi.
    Share on Google Plus

    About MWERA AMAZING

    This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
      Blogger Comment

    0 maoni:

    Post a Comment