MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

Trump aionya vikali Korea Kaskazini kuhusu makombora

Baada ya Korea Kaskazini kurusha makombora, majirani wao Korea Kusini walianza kupeleza vivaru hivi viitwavyo howitzers, karibu na mpaka wa mataifa hayo mawiliHaki miliki ya pichaEPA
Image captionBaada ya Korea Kaskazini kurusha makombora, majirani wao Korea Kusini walianza kupeleza vivaru hivi viitwavyo howitzers, karibu na mpaka wa mataifa hayo mawili
Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa hatua ya hivi punde Korea Kaskazini ya kurusha makombora yake ni ishara kuwa "ni uchokozi wa wazi" dhidi ya majirani zake na kinyume na sheria za Umoja wa Mataifa.
Amesema kuwa Korea Kaskazini itazidi kutengwa zaidi, na kwamba ''mbinu zote ziko mezani' ambazo zinaweza kutumika dhidi ya Korea Kaskazini ikiwemo pia kutumia jeshi.
Kombora hilo lilipita juu ya anga ya kisiwa cha Hokkaido huko Japan na kuanguka ndani ya bahari ya Pasifiki.
Pyongyang inasema kuwa, hatua hiyo inatokana na uchokozi wa wazi wa mazoezi ya kijeshi kati ya Marekani na Korea Kusini, ambayo inasema ni zoezi la kijeshi tayari kuishambulia.
Urusi na China pia inaona mazoezi hayo kama kiini cha taharuki inayoshuhudiwa hivi sasa katika eneo hilo.
Njia iliyopitia kombora la Korea Kaskazini
Baraza la usalama la Umoja wa mataifa inajiandaa kufanya mkutano wa dharura, kutokana na swala hilo.
Kabla ya kufanyika kwa mkutano huo, katibu mkuu wa Umoja wa mataifa, Antonio Guterres, amesema kwamba, kurushwa kwa makombora hayo kunahujumu udhabiti na hali ya usalama wa eneo hilo.
Ameitaka Pyongyang kufuata kwa dhati majukumu na sheria za kimataifa.
Kwa njia ya taarifa aliyoitoa Rais Donald Trump wa Marekani katika Ikulu ya White House, amesema kuwa "ameipokea vizuri mno ujumbe wa hivi punde wa Korea Kaskazini".
"Utawala huu imeonyesha bayana uchokozi wa wazi dhidi ya majirani zao, wanachama wote wa Umoja wa Mataifa na hali yake haijali kabisa tabia na namna mataifa mengine ya dunia yalivyo," alisema.
'Kitu kingine ambacho tulisikia, ni king`ora kuzima'
"Vitisho na tabia ya kuhujumu usalama, inaongeza hatari ya taifa hilo kutengwa zaidi, na kati ya mataifa yote duniani, kila mbinu ya kutumika iko wazi mezani."
Mapema mwezi huu, Rais Trump aliionya Pyongyang kuwa "itakabiliwa moto na ghadhabu" ikiwa itaendelea kutoa vitisho kwa Marekani, huku Korea Kaskazini nayo ikaitisha Marekani kuwa itarusha makombora makali na kushambulia kisiwa chake cha Guam, kilichoko katika bahari ya Pasifiki.
Hata hivyo, balozi wa Korea Kaskazini katika umoja wa mataifa, Han Tae-Song, amesema kuwa taifa lake lina haki ya kujibu mazoezi hayo yanayoendelea ya kijeshi.

KUTOKA BBC SWAHILI
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment