SUDANI KUSINI NA SUDAN ZAFIKIA MWAFAKA
Sudan
na Sudan Kusini zimeafikia makubaliano kuhusu mgogoro
wa
mpaka na uzalishaji wa mafuta.
Baada
ya mazungumzo ya siku ya nne, nchi hizo mbili zimeafikianakuruhusu usafirishaji wa mafuta kutoka kusini kupitia mabomba ya
Kaskazini na kuondoa wanajeshi mpakani.
Viongozi wa nchi hizo mbili hatimaye walikubaliana baada ya
mazungumzo ya siku nne mjini Addis Ababa Ethiopia.
Lakin maswala kadhaa muhimu yangali kutatuliwa ikiwemo
kuafikia makubaliano kuhusu mipaka inayozozaniwa ikiwa ni
mojawpao ya kilichosababisha mgogoro ambao nusura utumbukize
nchi hizo kwenye vita mapema mwaka huu.
Baada ya mapigano kuzuka kuhusu mzozo wa mafuta na mipaka,
Umoja wa mataifa ulitishia kuziwekea pande zote mbili vikwazo
ikiwa hazitaafikia makubaliano ya kina.
Wapatanishi wa Muungano wa Afrika wangali kuthibitisha kuwa
makubaliano yameafikiwa lakini rais wa Sudan Omar al-Bashir na
mwenzake wa Kusini Salva Kiir, wanatarajiwa kutia saini
makubaliano hayo hii leo.
Maelezo yametolewa tu kwa mukhtasari lakini wapatanishi
wa pande zote mbili, walisema kuwa wamekubaliana kuhusu eneo la
nchi hizo mbili ambalo halina ulinzi wa kijeshi.
Pia makubaliano ya kiuchumi yaliafikiwa kuruhusu Sudan Kusini
kuanza tena shughuli zake za kuzalisha mafuta.
Lakini mwafaka haukupatikana kuhusu eneo linalozozaniwa la Abyei
wala mipaka mingine mingi ambayo nchi hizo zinazozania.
Kwa hivyo makubalino hayo hayajaweza kutimiza masharti ya
Umoja wa Mataifa kwa nchi hizo kuafikia mkataba unaotatua mzozo huo kwa kina

0 maoni:
Post a Comment