AFUENI KWA WANAFUNZI WA KENYA
Shule za umma nchini Kenya
zimefungua hii leo baada ya wiki tatu
za mgomo wa walimu.
Walimu hao hatimaye waliweza kuafikia
makubaliano na serikali kuhusumatakwa yao ya nyongeza ya mishahara.
Serikali ilitishia kuwafuta kazi walimu hao Ijumaa wiki jana wakati walipokataa pendekezo la asilimia 4 ya mishahara ambalo serikali ilitoa.
Lakini makubaliano hatimaye yaliafikiwa mwishoni mwa wiki ya nyongeza ya asilimia arobaini.
Sasa mwalimu atakayepokea mshahara mdogo zaidi kuliko wote atalipwa dola 140 huku mwenye kulipwa mshahara mkubwa akipata dola 1,700 .
0 maoni:
Post a Comment