MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG
                            WASOMALI WA NAIROBI WASHAMBULIWA

Kundi lilokuwa na hasira limewashambulia Wasomali katika mtaa wa Eastleigh, Nairobi, baada ya guruneti kurushwa kwenye shule ya Jumapili ya watoto wa Kikristo, na kuuwa mtoto mmoja na kuwajeruhi kadha.
Polisi wakilinda mtaa wa Nairobi

Polisi waliwatawanya vijana ambao waliwalenga Wasomali wa mtaa wa Eastleigh.

Polisi wanasema watu 13 walijeruhiwa katika mashambulio hayo ya kulipiza kisasi.

Katika mashambulio ya karibuni dhidi ya makanisa nchini Kenya, wamelaumiwa wapiganaji wa Kiislamu, al-Shabaab wa Somalia, ambako wanajeshi wa Kenya wakishirikiana na wale wa Umoja wa Afrika wanapambana na wapiganaji hao.
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment