WANAFUNZI
20 WAUAWA NA BOKO HARAM
Takriban
wanafunzi 20 wameuawa kwa kupigwa risasi katika eneo
la Mubi, Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Polisi
wamefahamisha BBC kuwa shambulizi hilo limetokea katika
dahalia ya wanafunzo(Hostel) mbali kidogo na
chuo cha ufundi anuwai
cha
Mubi.
Mhadhiri
mmoja amefahamisha BBC kuwa wanafunzi 40 wameuawa
lakini
bado taarifa hizo hazijathibitishwa.
Mauaji
haya yanakuja siku chache baada ya operesheni kali kufanywa
dhidi
ya kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Boko Haram mjini humo.
Aidha
mhadhiri ambaye hakutaka kutajwa, aliambia BBC kwamba
wanafunzi
waliamrishwa kupanga foleni na kusema majina yao mmoja
baada ya mwingine kabla ya kuuawa.
Haijulikani
kwa nini baadhi waliuawa na wengine kuachwa, baadhi
ya
wale waliouawa ni waisilamu.
"kila
mtu anaogopa na wamejifungia vyumbani," alisema mhadhiri huyo.
Aliongeza
kuwa wanafunzi sasa wameanza kuuhama mji huo.
Inasemekana wameweka majani ya rangi ya kijani
kibichi kwenye
magari
yao kama ishara kuwa hawaungi mkono upande wowote.
Wapiganaji
wa Boko Haram wanaopigana wakitaka sheria za kiisilamu
kutumika,
wamewaua zaidi ya watu 1,000 Kaskazini mwa Nigeria.

0 maoni:
Post a Comment