Polisi nchini Ghana
wanawahoji wazazi walioshtakiwa kwa kuwafungia nyumbani wanao walio kati ya
umri wa miaka minne na minane tangu kuzaliwa kwao.
Polisi walivamia makao
yao yenye vyumba vinne mjini Accra,siku ya Ijumaa na kuwaokoa watoto hao ,
mvulana mmoja na wasichana wawili.
Wazazi hao waliwaambia
polisi kuwa hawakutaka kuwatoa wanao nje kwa hofu ya kukusanyika na watu waovu.
Watoto hao sasa
wamepelekwa katika makao ya kuwatunza watoto huku kukiwa na hofu kuwa wazazi
wao huenda ni wagonjwa wa akili.
Mwandishi wa BBC mjini
Accra anasema kuwa kisa hicho kimewashangaza sana watu mjini humo.
Inaarifiwa watoto hao
walifungiwa nyumbani tangu kuzaliwa kwao na hawamkujua yeyote isipokuwa wazazi
wao.
Aidha watoto hao
waliishi katika chumba kimoja, huku Kondoo na kuku wakiwa katika vyumba viwili
huku wazazi wao wakilala katika chumba chao kwenye nyumba hiyo iliyikuwa imejaa
uvundo.
Nyumba ilionekana kama
isiyoishi watu na licha ya kuwa haikuwa imesafishwa kwa miaka mingi, kuta zake
zilikuwa na michoro.
Polisi walivamia
nyumba hiyo baada ya jirani mmoja mwenye shauku kuwaarifu .
Wazazi wa watoto hao
wanahojiwa na polisi pamoja na madaktari wa magonjwa ya kiakili mjini Accra,
huku watoto hao wakipewa malezi na familia moja.
Msemaji wa polisi
alisema kuwa wazazi wa watoto hao hawakuwahi kuruhusiwa kutoka nje ya nyumba
yao.
Watoto waliwaarifu
polisi kuwa baba yao ambaye hakuwa na ajira, aliwasomesha hesabu na kiingereza
nyumbani kwao
Kkutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment