Mkuu wa Jeshi la Misri amewataka
wananchi kujitokeza kuandamana siku ya Ijumaa dhidi ya kile anachokiita ugaidi.
Abdel Fattah al-Sisi amesema
anawataka watu kuunga mkono jeshi na kulikabidhi jukumu la kukabiliana na
ghasia pamoja na ugaidi.
Wafuasi wa Mohammed Morsi
aliyeondolewa mamlakani na jeshi, wamekuwa wakiandamana dhidi ya jeshi ambalo
lilimuondoa mamlakani tarehe 3 mwezi Julai.
Lakini Generali Sisi alisema wito
wake sio wa ghasia bali anataka kuwepo maridhiano ya kitaifa.
"Ninawasihi watu kuandamana
Ijumaa hii kuthibitisha kuwa wananipa mamlaka mimi na jeshi langu kukabiliana
na ghasia pamoja na ugaidi,'' alisema Generali Sisi ambaye pia ni waziri wa
ulinzi katika serikali mpya.
Alikuwa anazungumza katika sherehe
za wanafunzi kufuzu chuo kikuu.
Alipinga madai ya migawanyiko
jeshini. ''Ninaapa kwa Mungu kuwa jeshi lina msimamo mmoja,'' alisema Sisi.
Akigusia hoja ya jeshi kumwondoa
mamlakani Morsi, alisema kuwa : '' nilimshauri Morsi kuwa rais wa wamisri
wote.''
Na akikumbuka uchaguzi wa urais wa
mwaka 2012, wakati Morsi alipochaguliwa, alisema kuwa aliwashauri wanachama wa
chama cha Brotherhood kutogombea uchaguzi huo, lakini wakampuuza.
0 maoni:
Post a Comment