Tanzania inapendekeza
kufanyiwa, marekebisho sheria ya kulinda amani, kuwezesha vikosi vya kulinda
amani kujikinga na mashambulizi.
Hii ni baada ya
walinda amani saba wa Tanzania kuuawa na watu waliokuwa wamejihami eneo la
Darfur mwishoni wa wiki.
Wanajeshi wengi
walijeruhiwa baadhi wako mahututi.
Mauaji ya walinda
amani 7 wa Tanzania nchini Sudan imewashangaza wengi sana nchini humo kulingana
na naibu waziri mkuu kwani nchi hiyo ndio imeanza kushika kasi katika juhudi
zake za amani kimataifa. .
Maafisa hawakuwa na
taarifa kamili kuhusu uvamizi wa Jumamosi ambapo wanajeshiu wengine 17
walijeruhiwa vibaya katika shambulizi baya zaidi kushuhudiwa dhidi ya vikosi
vya kimataiofa nchini Sudan.
Shambulizi hilo
lililofanywa na kikundi kikubwa cha watu waliokuwa wamejihami, ilihusisha
mashambulizi makali ya mizinga na iliyolenga wanajeshi hao umbali wa kilomita
25 Magharibi mwa mji wa Khor Abeche.
Tanzania, ambayo
pakubwa ni nchi salama na thabiti katika Kanda ya Afrika Mashariki, imeendelea
kujitolea sana katika juhudi za amani duniani.
Mwaka jana ilikuwa
nchi ya kwanza kujitolea kupeleka vikosi vyake Mashariki mwa Congo, chini ya
kile ambacho kitakuwa kikosi cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa wenye jukumu
la kupambana vilivyo na makundi ya waasi huko.
Kutoka BBC.
0 maoni:
Post a Comment