Serikali ya afrika Kusini
imekanusha taarifa za vyombo vya habari kwamba aliyekuwa kiongozi wa afrika
Kusini, Nelson Mandela, ambaye amelazwa hospitali tangu mwezi wa Juni, kwamba
alirejeshwa nyumbani Johannesburg Ijumaa usiku.
Taarifa ya serikali imesema kuwa Bwana
Mandela bado yuko hospitali mjini Pretoria na kwamba bado mahtuti, lakini hali
yake imetulia.
Kulazwa kwa muda mrefu kwa kiongozi huyo
kumewatia wasiwasi raia wa taifa hilo na ulimwengu kwa jumla.
Mandela ambaye ana umri wa miaka 95,
alikuwa Muafrika wa kwanza kuwa rais wa taifa la Afrika Kusini, na anaheshimiwa
na wengi kama baba wa taifa.
Kutoka BBC.
0 maoni:
Post a Comment