Aliyekuwa Rais wa
Afrika Kusini Nlson Mandela amemaliza siku moja nyumbani kwake Johansberg
baadha ya kuondoka hospitalini alikokuwa amelazwa kwa zaidi za miezi mitatu
akipokea matibabu kwa maambukizi ya mapafu anayougua.
Nelson Mandela kwa
sasa anendelea kupata nafuu nyumbani. Serikali ya Afrika Kusini imesema atakuwa
akipata huduma sawa za zile alizokuwa akipewa hospitalini jijini Pretoria.
Maafisa wa serikali
wameongezea kuwa nyumba yake imekarabatiwa kuwezesha madakatari kumtibu akiwa
humo. Madakatri wataalam ambao wamekuwa wakimshughulikia wataendela kumtibu
nyumbani mwake, lakini ikiwa hali yake ya afya itahitaji huduma za hospitali
basi atarejeshwa humo bila kuchelewa.
Inasemekana kurudi
nyumbani kwa Mandela kumetia matumaini kwa familia yake pamoja na taifa la
Afrika Kusini. Hata hivyo Mzee Mandela bado anaonekana mwenye afya dhaifu.
Serikali ya Afrika
Kusini ilisema hapo jana kuwa Mandela, alitolewa hospitali ambako amekuwa
akitibiwa mapafu tangu mwezi Juni.
Taarifa katika tovuti
ya rais wa Afrika Kusini ilieleza kuwa Bwana Mandela bado ni mahtuti na hali
yake wakati mwengine inabadilika.
Lakini madaktari wake
wanaamini akiwa nyumbani kwake mjini Johannesburg atapata matibabu sawa na yale
ya hospitali.
Serikali imesema
inamtakia mema wakati akiendelea na matibabu.
Kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment