Pambano
la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya wenyeji Ruvu Shooting na Simba
lililochezwa jana (Oktoba 5 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
imeingiza sh. 75,692,000.
Watazamaji
waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo namba 43 la VPL msimu wa 2013/2014
lililomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 walikuwa 13,395.
Viingilio
katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku
kila klabu ikipata mgawo wa sh. 17,983,902.31 wakati Kodi ya Ongezeko la
Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 11,546,237.29.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 9,144,357.11, tiketi sh.
3,183,382, gharama za mechi sh. 5,486,614.26, Kamati ya Ligi sh. 5,486,614.26,
Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,743,307.13, Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) sh. 1,066,841.66 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa
wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,066,841.66.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 maoni:
Post a Comment