MR.Blue |
MR. Blue, amekanusha kufanya utapeli
nchini Kenya kama ilivyoripotiwa katika vyombo vya Habari likiwemo Gazeti Moja
nchini Kenya na mitandao ya Kijamii, amesema kuwa kuna mtu anayetumia jina lake katika
kutapeli watu.
Mr – Blue amesema kuwa ameshangazwa na kitendo cha
kusemwa kuwa amefanya utapeli nchini Kenya “ sikuwa na show Kenya wala nini, ni
waongo tu, kuna jamaa aliniambia kuna mtu amemlipa hela kwaajili ya kufanya
show Kenya, ambaye anajiita Mr.Blue halafu hajatokea , mimi nimewaambia
wametapeliwa na watu wa kwenye mitandao, kama wana uhakika ni mimi waje
kunikamata nyumbani.” Hayo yalikuwa maneno ya Mr Blue alipokuwa akifanyiwa
mahojiano na Bongo5.
Aliendelea kwa kusema kuwa “ hauwezi kufanya show nje
ya nchi bila kuwa na mkataba , na kama wao wana mkataba na mimi nimechukua
kiasi cha pesa kwaajili ya show, basi waanike hadharani watu waone”
0 maoni:
Post a Comment