Watoto wa P Diddy. |
Watoto wa Rapper P DIDDY, wamejitolea kusaidia wahanga wa kimbunga
kilichotokea Ufilipino kilichosababisha watu na mali zao kupotea.
Watoto wa Diddy, wameguswa na tukio hilo na kuamua kujitolea msaada kwa wahanga
wa Kimbunga hicho.
Watoto hao wameamua kukusanya nguo, viatu vyao pamoja
na mablangeti na kuvituma nchini Ufilipino kwaajili ya kuwasaidia watu hasa
watoto wenzao waliokumbwa na majanga hayo.
Inadaiwa kuwa P diddy ni kati ya wazazi wenye
mafanikio makubwa pia ni mmoja kati ya wazazi wanaolea watoto katika misingi bora
ya kujua umuhimu wa kusaidia watu wengine hasa wenye mahitaji makubwa kwenye
kipindi kigumu kama hichi kwa wafilipino.
0 maoni:
Post a Comment