Maafisa wakuu nchini Misri wamesifu sana idadi kubwa ya watu waliojitokeza
kupigia kura ya maamuzi katiba mpya........
Jeshi limekuwa likiwashawishi watu kupiga kura ya ndio
ili kuhalalisha kuondolewa mamlakani kwa aliyekuwa Rais Mohammed Morsi.
Afisa mmoja mkuu wa uchaguzi, Nabil Salib,ameambia
vyombo vya habari kwamba idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura ya maamuzi
ilikuwa kubwa sana
kinyume na matarajio ya wengi.
Siku ya pili ya kura hiyo ambayo ilikuwa Jumatano
ilikamilika kwa Amani .
Watu tisa waliuawa Jumanne kwenye mapigano kati ya
makundi mawili hasimu yakiwahusisha wafuasi wa Morsi.
Polisi waliwakamata watu 400 katika siku mbili za
kwanza za kura hiyo ambao walidaiwa kusababisha vurugu wakati wa shughuli hiyo.
Afisaa mmoja mkuu katika wizara ya mambo ya ndani,
alinukuliwa akisema huenda idadi hiyo ilifika asilimia 55 ya wapiga kura.
Matokeo ya mapema yanaonyesha kuwa katiba hiyo
imekubalika kwa asilimia 95.
Hata hivyo, wanachama wa vuguvugu la Muslim
Brotherhood walisusia kura hiyo.
Matokeo ya kura hiyo huenda yakatolewa Ijumaa.
kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment