Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, amesema kuwa jeshi la
Uganda linashirikiana na
wanajeshi wa Sudan kusini
kupambana na waasi wa Sudan
Kusini........
Mapigano hayo ambayo yalizuka mwezi uliopita
yanaendelea katika maeneo kadhaa ya Sudan kusini, licha ya kufufuliwa kwa
mazungumzo ya amani katika nchi jirani ya Ethiopia .
Mkutano wa kupatanisha makundi yanayozozana Sudan Kusini unaendelea nchini Ethiopia |
Baada ya wiki kadhaa za tetesi za wanjeshi wa Uganda
kuwa nchini Sudan Kusini, jeshi la Uganda
sasa limekiri rasmi kuwa liko katika vita na waasi wa Sudan Kusini.
Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi, Luteni Kanali Paddy
Ankunda, Uganda
ina takriban wanajeshi elfu moja na mia sita nchini humo.
0 maoni:
Post a Comment