Wanamgambo wa kiislam nchini Somalia wameshambulia hoteli moja muhimu katika
eneo la Kati mwa Somalia
ambalo wanamgambo hao walipoteza udhibiti wake wiki iliyopita...........
Walioshuhudia shambulio hilo
wameiambia BBC kuwa gari lililipuka nje ya hoteli hiyo katika mji wa Bulo-burde
wanakoishi askari wa muungano wa Afrika na makamanda katika jeshi la Somalia .
Mlipuko huo ulifuatiwa na makabiliano ya risasi
yaliyodumu kwa muda wa saa tano .
Walioshuhudia wanasema takriban watu kumi na wanne
wameuawa katika shambulio hilo , ambalo wapiganaji wa al-Shabab wamesema
walilitekeleza.
Mji wa Bulo-burde ulitwaliwa tena katika moja ya
harakati za kijeshi zinazoendeshwa na vikosi vya Amison na vile vya serikali
dhidi ya wanamgambo hao.
kutoka BBC.
0 maoni:
Post a Comment